Msanii
Rose Ndauka amesema kitendo cha msanii Harmonize kujibu majibu yenye
utata alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na
East Africa Televisio, hakupendezwa nacho kwani kinazidi kuleta
sintofahamu.
Rose
Ndauka ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na
East Africa Radio, na kusema kwamba Harmonize alitakiwa kujibu moja
kwamoja kuwa hawana mahusiano yoyote zaidi ya kufahamiana nae kikazi.
“Mi
Harmonize namfahamu kama msanii, na hii issue sio mara ya kwanza,
tayari nilishaona alihojiwa kwenye interview nyingine alihojiwa kuhusu
mimi, what I didn't like ni kwamba angeongea straight, unajua kama huna
mahusiano na mtu na ukaulizwa unaongea moja kwa moja, kitendo cha
kutengeneza mazingira na watu wakaanza kuweka doubt kwamba Rose na
Harmonize watakuwa na mahusiano, hicho ni kitu ambacho mimi
sikukipenda”, alisema Rose Ndauka.
Rose
Ndauka aliendelea kwa kusema kwamba yeye na Haronize hawana mahusiano
kama ambavyo Harmonize alielezea, na kwamba iko tofauti na watu
wanavyofikiria.
“The
way alivyolijibu ilo suala kwamba mimi na yeye tunafahamiana kwamba
naongea nae sana, mi na Harmonize hatuongei sana, na hata kama tunaongea
labda Rose naomba nipostie hiki, sio kwamba ni mtu ambaye namfahamu
sana au tuna mahusiano ya karibu sana, iko tofauti sana na yeye
alivyojibu”, alisema Rose Ndauka.
Wiki
iliyopita Harmonize alihojiwa kuhusu uhusiano wake na Rose Naduka
kwenye kipindi cha Planet Bongo baada ya kuonekana wana ukaribu sana, na
kutoa majibu ambayo yalileta sintofahamu kwa jamii.
EATV.TV

No comments:
Post a Comment