Mama wa staa wa muziki Bongo, Sanura Kassim ‘Sandra’.SINEMA limeanza!
Sanura Kassim ‘Sandra’ ni mama mzazi wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni anadaiwa kuingia katika figisufigisu na
mwanaye huyo kwa kumuhoji kama kweli Latiffah ‘Tiffah’ ni damu yake kwa
kumzaa na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Amani limenyetishiwa.
Akizungumza
na mwandishi wetu Jumatatu ya wiki hii, mmoja wa wanandugu wa Diamond
alisema ishu hiyo ilijiri hivi karibuni nyumbani kwa Diamond, Madale
jijini Dar ambapo mama na mwana hao walikuwa katika mazungumzo ya
kawaida.
Ndipo, mama Diamond alipojikuta akiponyokwa na sentensi hiyo ya
kuhoji uhalali wa Tiffah kuwa mtoto wa Diamond kauli ambayo awali
ilichukuliwa kama utani wa bibi na mjukuu!
‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.‘Yuda’ huyo wa
Diamond, alizidi kusema kuwa, mama huyo alijikuta akimtaka Diamond
aachane na wazo la kumhesabu Tiffah kama mwanaye kwani hafanani naye
hata kidogo na kwamba ameuziwa mbuzi kwenye gunia kama si mfuko wa
chumvi!
“Diamond alibadilika sura na kumtaka mama yake aachane na utani wa
namna hiyo. Lakini mama alisisitiza kuwa si utani bali ni ukweli ambao
amekuwa akivizia autoe kwa njia gani, hivyo siku hiyo aliona ndiyo muda
mwafaka wa kutoa la moyoni.
“Kaka (mwandishi), ilibidi Diamond aondoke pale maana anampenda sana
mama yake na huwa hapendi kumuudhi. Hivyo ili kuepusha mambo mengine,
aliamua kwenda chumbani kwake. Lakini mama haikuishia hapo, alimfuata na
kugonga mlango huku akisisitiza juu ya suala hilo.
“Sasa ninavyoongea na wewe, Diamond ana kama siku mbili au tatu
hajaonekana nyumbani, anamkwepa mama yake maana naye amekomaa akimtaka
mwanaye amuweke wazi anachofahamu kuhusu uhalali wa Tiffah kuwa damu
yake,” alisema mtoa habari huyo ambaye ombi lake kubwa kwa mwandishi
wetu ni hifadhi ya jina lake ili kuepuka kuonekana ni ‘kikulacho’ cha
familia hiyo.
Kama kawaida ya gazeti hili, ambalo ni mashine
bab’kubwa kwa habari za ndani za mastaa wa Bongo, kujiridhisha na kila
habari kabla ya kuichapisha na kuipeleka kwa msomaji, ‘kiranja mkuu’ wa
dawati alimtafuta mama huyo kupitia simu yake ya mkononi ambapo
aliposomewa madai hayo mpaka mwisho, aliishia kusema:
“Jamani, kwanza mimi naumwa! Sitaki kabisa maswali magumu kiasi hicho
cha kuumiza kichwa, niacheni na familia yangu,” (akakata simu na
kuizima).
Amani lilimsaka Diamond mwenyewe kwa njia ya simu kwa kumtumia meseji na ilimfikia (deliva) lakini hakujibu kitu.
Agosti
mwaka huu, Zari alimzalia Diamond mtoto huyo na kuibua hisia tofauti
kutoka kwa wadau, hasa wa nchini Uganda ambako Zari ana asili nako,
wakidai mtoto huyo si wa Diamond.
Hata hivyo, Diamod amekuwa akisema Tiffah ni mtoto wake na ana uhakika na hilo.
GPL
This article:
Mama Diamond Ambana Diamond Kuhusu Uhalali wa Mtoto Latiffah Katika Familia Yao..Mengi Yasemwa Mtaani
hajizjini
VIDEO
Mama Diamond Ambana Diamond Kuhusu Uhalali wa Mtoto Latiffah Katika Familia Yao..Mengi Yasemwa Mtaani
Mama Diamond Ambana Diamond Kuhusu Uhalali wa Mtoto Latiffah Katika Familia Yao..Mengi Yasemwa Mtaani
Reviewed by AfricanForum
on
November 26, 2015
Rating: 5
Reviewed by AfricanForum
on
November 26, 2015
Rating: 5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment