Mshindi wa tuzo ya Muongozaji Wa Video Anayependwa katika Tuzo Za Watu 2014, director Nisher amefunguka kwa kirefu mambo mbalimbali kuhusu ukimya wake.
Unauzungumziaje
mwaka 2015 kwako kwasababu umefanya video chache tofauti na matarajio
ya wengi waliodhani baada ya kushinda tuzo ungefanya makubwa zaidi
Nisher:
Mwaka 2015 nilijua utakua na changamoto zaidi sababu options
(ma-director) zimekua nyingi zaidi na wasanii walishaanza kutaka
kuonekana zaidi Afrika badala ya East Africa tu, so Kukatokea MASHINDANO
ambayo ndio yanayoendelea mpaka sasa, ikapelekea safari za wasanii nje
ya TZ kua nyingi, hii ikalazimu Directors wote wa nyumbani kushusha bei
za video ili wasikose wateja, kitu ambacho kwa directors wakubwa ni
mmomonyoko wa biashara sababu kushuka kwa bei inamaanisha huwezi fanya
kazi kubwa kwa budget kubwa kama zamani na huwezi kufanya usambazaji
kwenye TV stations za nje sababu hizo process zinataka fedha za
ufuatiliaji!!!
So
wasanii wengi Wa class A nchini wote waliona ni bora kufanya kazi nje
kuliko ndani sababu nje watalipa hela ya video na hiyo hiyo itasambaza
kazi kuliko kutulipa sisi wa nyumbani wakisahau kua wanatumia nauli za
ndege na hela za hotels ambazo wangeweza kusave wakafanya kazi bora tu
nyumbani!!!
Kitu
nimejifunza ni kwamba wasanii wengi husema directors wa nyumbani
wasumbufu na hawathamini kazi za wasanii, hili pengine likiwa ni kweli
na sio kweli maana binafsi nadhani ni kuutambua wakati tu na kujua kua
hii ni biashara! Huu Ni wakati wa Tanzania kushine, na kwenda
international zaidi, ila kama budget haziruhusi mtu kama mimi siwezi
kujikaza ili niwe na video Kwenye market ili nipate attention wakati
HAINILIPI, bora nifanye kazi zingine kwanza then wasanii wakija kuona
wanatumia hela sana nje wakaamua kurudisha nguvu nyumbani ni rahisi
kurejea!!! Ila haya mashindano wanayoyafanya Kumuiga Diamond kua kama
yeye watayafanya mwishowe watachoka….. Kila mtu ana nyota yake kwenye
hii industry…. Huwezi Fanya hii biashara kwakuiga flani anafanya nini na
wewe ndo ufanye utafika mahali utachoka na hela haitakuruhusu!!!!
Kwa
muda huu uliokaa kimya ni kitu gani unajishughulisha nacho mbali na
kushoot video? Na ukimya huu hauoni kama unaweza kuwa na athari kutokana
na ukweli kwamba kadri unavyoendelea kuwa kimya ndio unavyozidi
kupotea?
Nisher:
Kwangu sioni vibaya kutulia na kuja kurudi when I feel the time is
right, jina langu ni kubwa tayari ni kama ndege yenye mafuta inasubiri
mvua mbaya ziishe inyanyuke!!!
Sasa
hivi nafanya biashara zangu Arusha, including music production, mwaka
huu nime produce kazi ya Fid Q ya ‘Bendera ya chuma’ ambayo aliiperform
live at #Cockestudioafrica, which hiyo was a big deal for me, Kuna
baadhi ya wasanii wananicheki kufanya kazi za video ila changamoto kwao
inakuja kwenye swala la hela, wakati wa malipo wanapotea, sitataja
majina ila ni wasanii wakubwa tu!
Kazi ya kuongoza video imeshakutengenezea pesa kiasi gani toka uanze?
Nisher:
Kiukweli through out my career kama director na music producer na kazi
zangu mbali mbali nje ya hizi fani nimetengeneza hela nyingi ambayo
nikisema sasa hivi nisifanye hii kazi tena bado nitakua fine kabisa!!…
This is why hata ninapopewa deal ya kazi napenda kuifanya nikiwa
comfortable na client wangu aridhike na kazi yake kwa asilimia
1000/100….. sitaki kufanyia njaa tena!!!
Ikiwa tunaelekea kuumaliza mwaka 2015 una waahidi nini mashabiki wako kwa mwaka ujao?
Nisher:
2016 siwezi yasema ya Mungu, mimi napanga Mungu anapanga pia… Ila
ninachojua for now I’m in a peaceful place in life, Sihitaji
kumfurahisha mtu yeyote duniani… Nimeishi maisha yangu miaka yote
nikipendeza watu tu nikasahau kujifanyia mema mwenyewe so kwasasa
najitendea wema kwanza!!!
Kitu
kimoja ninacho waahidi Mashabiki wangu wale waukweli sio wale wakupita
Ni kwamba Nitarudi tena na Nitawafurahisha Zaidi kuliko hata mwanzo,
isipokua wawe na subira tu, Movie kali haitaki haraka!!!!
NISHER WILL BE BACK, WHEN READY!!!
hajizjini
VIDEO
Director Nisher Afunguka Mengi Kuhusu Ukimya Wake na Changamoto Alizopata !
Director Nisher Afunguka Mengi Kuhusu Ukimya Wake na Changamoto Alizopata !
Reviewed by AfricanForum
on
November 26, 2015
Rating: 5
Reviewed by AfricanForum
on
November 26, 2015
Rating: 5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment