Kila kitu ukizidisha ni sumu! Ndivyo ilivyotokea kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye anadaiwa kumtupia lawama mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuwa amemharibu mtoto wao, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kwa kumzidishia vikorombwezo vya urembo, Ijumaa Wikienda limetonywa.
The
Boss Lady.Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho ni ‘memba’ wa
familia ya Diamond au Dangote au Chibu zilieleza kwamba, kitendo cha
Zari kumpodoa Tiffah kupita kiasi kimekuwa kikimpa shaka jamaa huyo
akihofia kuwa kinaweza kumsababishia mwanaye kilema.“Unajua mwanzoni Zari alianza kwa kumpaka lipstick na kumchora wanja lakini Diamond hakuona ni ishu sana.“Lakini Zari alipoanza kumwekea mawigi na kope za bandia, ndiyo jamaa akashtuka na kuanza kuuliza kama zina madhara au hazina?

No comments:
Post a Comment