“Nimesaidia wengi sana kwenye huu muziki toka zamani, akina AT, Berry Black, akina Bella, Ray C , Mzee Yusuf,” alisema.
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Mzee Yusuf anakuja kwenye studio yangu alikuwa anataka arekodi wimbo wa Hip Hop mimi nikamwambia wewe unafaa kwenye mduara ndio akaanza kurekodi nyimbo za mduara na mimi ndiye niliyemfanyia album yake ya kwanza. Kwahiyo mimi ni miongoni mwa watayarishaji wa zamani ambao tuliweza kuwashape wasanii wengi mpaka leo hii unaona wanafanya fanya vizuri,” aliongeza.
Mtayarishaji huyo amesema kuwa sasa anajiweka sawa ili aje kivingine kwani anaamini kuwa bado ana nafasi kubwa katika muziki huu.
No comments:
Post a Comment