MADAI! Ndoa ya gwiji katika tasnia ya uigizaji na ushereheshaji
(MC)Bongo, Mahsein Awadhi Said ‘Dokta Cheni’ inadaiwa kushikiliwa na
‘uzi wa buibui’ kufuatia mwigizaji huyo kukolea kwa mchepuko anayedaiwa
kumpangishia chumba katika hoteli moja maarufu jijini Dar, Amani
linaripoti.
Kama ilivyo kwa Rais, Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
Jumatatu iliyopita, paparazi wetu alifanya ‘ziara’ ya kushtukiza katika
hoteli hiyo ambayo inadaiwa msanii huyo kampangishia chumba mwanamke
huyo (jina lipo) ambaye pia ni msanii wa filamu.
Mwandishi wetu alipoomba kuonana na msanii huyo, hakupata ushirikiano wa
kutosha kutoka kwa wahudumu wa hoteli na kuamua kumtafuta Dokta Cheni
kwa njia ya simu ambaye alidai yupo ‘lokesheni’ katika hoteli hiyo.
Aliposomewa madai hayo, akafunguka hivi:
“Unajua mambo hayo yanavumishwa na watu wasioitakia mema ndoa yangu. Ni
kweli kulikuwa na kasoro ndogondogo na mke wangu, lakini chanzo si
msichana, kuna baadhi ya wasanii wanajua ukweli huo.
“Hapa tuko kambini kwa ajili ya kuandaa filamu yangu mpya na kila siku
mke wangu anapita hapa. Sasa mambo kama hayo sielewi yanatoka wapi.
Ugomvi ulikuwa zamani sana,” alisema Dokta Cheni.
Jitihada za kumtafuta mke wa Dokta Cheni, Sabrina ziligonga mwamba kufuatia simu yake ya mkononi kutopatikana hewani.
Gwiji katika tasnia ya uigizaji Bongo, Mahsein Awadhi Said ‘Dokta Cheni’.
No comments:
Post a Comment