Sasa hivi kitu kipya kutoka kwa Jux ni audio na video ya One More
Night. Jux akiongea na Nick J Music Media amesema kwamba ameamua kuimba
ngoma ya mapenzi kwa idea ambayo hajawai kutumia hapo zamani. Akielezea
kuhusu alichoimba kwenye wimbo huo alisema hivi, “Mimi
nimekutana na msichana ninaye muimbia mara moja tu. Sasa baada ya hapo
msichana hakutaka tena uhusiano na mimi, lakini mimi natamani tuendelea
au itokee One More Night kama ile ya mwanzo”Kama ulikua hujui ni kwamba wimbo huu Jux ameandikiwa na Walter Chilambo, “Walter ameandika wimbo huu na mimi nilitaka kufanya kitu cha tofauti kabisa, kama kawaida tumekuta beat na Walter alikua na idea ya kuandika wimbo wa aina hii. Kwasababu nimeandika sana ngoma zangu mimi mwenyewe, sasa hivi nilitaka kujaribu kitu kipya, so kuanzia uandishi hadi melody ni kazi ya Walter Chilambo”, alisema Jux
Video yenyewe ni hii hapa.
No comments:
Post a Comment