Latest News

hajizjini

VIDEO

Wazee wa kimila wawatisha waliofukuliwa Nyangalata

Wazee wa kimila wa makabila ya Wakurya na Waluo wamesema watu watano waliookolewa kutoka kwenye machimbo ya Nyangalata, Kahama ambao waliwekewa matanga kabla ya kuibuka wanatakiwa kufanyiwa mambo ya kimila, vinginevyo watakufa kiajabu.


Mmoja wa wazee hao, Ghati Ryoba (61) wa Mtaa wa Mwangaza, Nyamisangura – Tarime alisema: “Mtu akidaiwa kuwa amekufa lakini baadaye akaonekana, wazee wa ukoo au wa mila humfanyia matambiko kama njia ya kuondoa mikosi kwake na kwa familia yake. Wanachukua kondoo mweusi wanamchinja kisha wanamtambikia (bharamsendola).

“Kisha wanachukua kinyesi cha kondoo (ubhuhu ghwaling’ondi) na mti mmoja unaitwa (richirya) kisha kile kinyesi kinarushwarushwa ndani ya nyumba yake na mji mzima kama kuna nyumba nyingine halafu wanachukua kile kinyesi cha kondoo na kumpaka kwenye mikono na anashikana mikono na watu.”
Mzee huyo wa kimila aliongeza kusema kuwa baada ya hapo atanawa mikono kabla ya kuruhusiwa kula na kujumuika na watu. Alisema baada ya hapo atanyolewa kisha atakwenda kuoga “... Wengine hupeleka nywele kuzizindika kwenye mlima ambako watu hawalimi.”
Kuhusu Waluo, mzee Peter Odello wa Kitembe, Rorya alisema: “Kama inatokea mtu anadaiwa kufa na watu wakafanya matanga lakini baadaye akaonekana, lazima arudi kijijini wamfanyie matambiko.”
Alisema akirudi, wazee watachinja ng’ombe na watu watakaa tena kama walivyokaa kwenye matanga kwa siku mbili au tatu watu wakila kisha kupewa dawa inayoitwa manyasi.

No comments:

Post a Comment

TAFUTA CHOCHOTE

KITAMBO

KITAMBO SANA

Recent Post

AUDIO