Uchapakazi wa Rais Dkt John Magufuli unatuma ujumbe si kwa maafisa wa
Tanzania pekee, bali na nchi za jirani pia na kuwaacha viongozi wa nchi
hizo kwenye wakati mgumu.
Kenya ambayo imekuwa ikifuatilia siasa za Tanzania tangu wakati wa
kampeni, imeonesha kupenda mbinu za Magufuli na wananchi wake wanatamani
mtu kama yeye.
Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Magufuli amefanya mambo makubwa na wananchi wamependa.
Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Muhimbili ilifichua uovu
mwingi na kupelekea kufutwa kwa bodi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo
na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto.
Ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za serikali kwaajili ya
kugharamia safari za nje za viongozi wa nchi, Magufuli aliamua
kuzisitisha mara moja.
Dkt Magufuli pia alielekeza kiasi cha shilingi milioni 225
zilichangwa kwaajili ya kugharamia hafla ya wabunge kupongezana mjini
Dodoma zipelekwe kwenda kununua vitanda. Badala yake shilingi milioni 15
pekee zilitumika kwaajili ya sherehe hiyo.
Siku chache baadaye vitanda hivyo na vifaa vingine vilinunuliwa na kupelekwa Muhimbili.
Jumatatu hii Magufuli alitangaza kuondoa sherehe za maadhimisho ya
siku ya Uhuru December 9 na fedha za maandalizi hayo zitumike kwa mambo
mengine muhimu.
Hayo na mambo mengine yamefanya Dkt Magufuli atrend nchini Kenya.
hajizjini
VIDEO
Uwezi Amini Rais Magufuli Awa Gumzo Kubwa Nchini Kenya…Watamani Awe Rais Wao…Wamkosoa Uhuru Kenyatta
Uwezi Amini Rais Magufuli Awa Gumzo Kubwa Nchini Kenya…Watamani Awe Rais Wao…Wamkosoa Uhuru Kenyatta
Reviewed by AfricanForum
on
November 24, 2015
Rating: 5
Reviewed by AfricanForum
on
November 24, 2015
Rating: 5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

This comment has been removed by the author.
ReplyDelete