Akizungumza leo,
Kamishna wa polisi Kanda Maalum wa Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema
Ulature ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mnandimkongo, wilayani Mkuranga
alikamatwa mwezi huu baada ya msako mkali wa polisi.
Kamanda Kova amesema
Ulature amejirusha kutoka ghorofa ya tatu katika jengo la makao makuu ya
polisi alipokuwa akihojiwa na maofisa upelelezi.
“Amejirusha kutoka
ghorofa ya tatu hadi chini baada ya kuaga kuwa anakwenda msalani,
tunadhani lengo la mtuhumiwa lilikuwa kujiua au kutoroka lakini yote
hayo hayakufanikiwa badala yake amejeruhiwa,” amesema kova
Amesema mtuhumiwa huyo amepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.
Kova amesema mtuhumiwa
huyo ndiye aliyekuwa `mchoraji’ wa matukio ya uvamizi katika vituo vya
polisi vya Ikwiriri, Kimanzichana na Stakishari ambako alisababisha
mauaji na uporaji wa silaha.
Amesema alikamatwa
katika kijiji cha Mamdimkongo ambako alikuwa akiishi kwa kujifichaficha.
Kamanda Kova amewashukuru wananchi kwa ushirikiano na kutaka waendelee
ili kukomesha matukio ya uhalifu kanda ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment